Sudani: Jeshi kuunda serikali ya mpito baada ya kuidhibiti Khartoum

Serikali ya Sudan inatarajiwa kuundwa mara baada ya kuudhbiti mji mkuu Khartoum, duru za kijeshi zimeliambia shirika la habari la REUTERS siku ya Jumapili, siku moja baada ya mkuu wa jeshi Abdel Fattah al-Burhan kutangaza hatua hiyo.

Imechapishwa:

Dakika 1

Matangazo ya kibiashara

Vyanzo vya kijeshi nchini Sudan vimeeleza kuwa serikali mpya inatarajiwa kuundwa baada ya kudhibitiwa kikamilifu kwa mji mkuu wa Khartoum.

FSR inatawala sehemu kubwa ya magharibi mwa nchi na inajaribu kuimarisha udhibiti wake katika eneo la Darfur kwa kuuteka mji wa el-Fashir. Jenerali Burhan amefuta wazo la kusitisha mapigano wakati wa mwezi mtukufu wa Ramadhani ikiwa RSF haisitisha mashambulizi yake.

Vita kati ya pande hizo mbili, vilivyozuka mwezi Aprili 2023, vimesababisha moja ya majanga makubwa zaidi ya kibinadamu duniani, huku zaidi ya watu milioni 12 wakikosa makazi na nusu ya watu wakikabiliwa na njaa.

“Tunaweza kuiita serikali ya mpito, serikali ya vita, ni serikali ambayo itatusaidia kufikia yale yaliyosalia ya malengo yetu ya kijeshi, ambayo ni kuikomboa Sudan kutoka kwa waasi hawa,” Jenerali Burhan alisema Jumamosi katika mkutano wa hadhara huko Port Sudan, ambako amekuwa na makao yake tangu kuanza kwa mzozo dhidi ya RSF.

Jenerali Burhan alisema mabadiliko yatafanywa kwa katiba ya mpito ya nchi hiyo ambapo vyanzo vya kijeshi vimesema yataondoa marejeleo yoyote ya ushirikiano na raia au RSF. Mamlaka itawekwa mikononi mwa jeshi pekee, ambalo litamteua waziri mkuu mwenye jukumu la kuteua baraza la mawaziri.

Abdel Fattah al-Burhan alitoa wito kwa wanachama wa muungano wa kiraia wa Taqadum kuachana na RSF