
Nchini Sudani, jeshi limetangaza kujiondoa katika eneo la mpaka na Misri na Libya baada ya kupigana na wanamgambo wa Vikosi vya Msaada wa Haraka vya Jenerali Hemedti. Jeshi la Sudani limemshutumu Jenerali Khalifa Haftar, mbabe wa kivita mashariki mwa Libya, kwa kutoa msaada wa kijeshi kwa RSF.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Kwa mujibu wa jeshi la Sudani, shambulio hilo lilifanyika mwishoni mwa wiki iliyopita kwenye mipaka ya Sudani, Libya na Misri. Kikosi cha Field Marshal Haftar-kinachojulikana kama Katiba Sobol al-Salam-kinachoendesha harakati zake kusini mwa Libya kilivuka mpaka na kuungana na wanamgambo wa RSF kushambulia eneo la jeshi la Sudan huko Jebel Uweina, zaidi ya kilomita tatu kutoka mpakani. Jeshi lilishutumu uchokozi wa wazi dhidi ya Sudani, unaolenga kuchukua udhibiti wa eneo hili la mpakani. Eneo la kimkakati kwa kuwa linatumika kama ukanda wa kusambaza silaha, mamluki na mafuta kwa RSF kutoka Libya.
Hii si mara ya kwanza kwa wapigaaji wa Khalifa Haftar kushirikiana na wanamgambo wa Hemedti, wote wakiungwa mkono na Falme za Kiarabu. “Daima kumekuwa na mamluki wa Libya wanaofanya kazi na wanamgambo wa Sudani, maafisa, mafundi wanaojua kuendesha ndege zisizo na rubani,” anabainisha mtafiti kutoka Sudani Magdi El Gizouli. “Lakini wakati huu, ni kikosi cha wapiganaji walioshiriki katika operesheni hiyo. Kikosi kinachomtii Haftar, na ambacho kwa kawaida kinahusika na usafirishaji wa silaha na hasa mafuta, kwa sababu huwezi kupigana huko Darfur bila kuwa na msururu wa usambazaji wa mafuta. Hiki kinatoka hasa Libya.” »
Mtafiti huyu anasema msaada wa kikosi cha Libya ulifidia ukosefu wa idadi ya kutosha ya wapiganaji wa vikosi vya Jenerali Hemedti. “Tatizo la RSF ni kuwa na uwezo wa kushikilia pande zote tofauti za vita. Wanataka kuendelea kuzingira El Fasher, na kufanya hivyo, ni lazima kudumisha mlolongo wa usambazaji,” mtafiti anaongeza. “Pia wanapigana huko Kordofan, ambapo wanakabiliwa na mashambulizi kadhaa ya jeshi. Hawana wapiganaji wa kutosha kwa pande zote hizi, na hawana muda wa kutosha wa kuwafunza wanajeshi wapya.”