
Mkuu wa jeshi la Sudani Jenerali Abdel Fattah al-Burhan amesema Jumatano jioni kwamba Khartoum “imekombolewa,” baada ya hapo awali kutangaza kwamba vikosi vyake vimeutwaa tena uwanja wa ndege wa mji mkuu, eneo la kimkakati na la kishara lililokaliwa tangu kuanza kwa vita na na Vikosi vya Msaada wa Haraka (RSF) vya Jenerali Mohamed Hamdane Daglo, anayejulikana kwa jina la Hemedti.
Imechapishwa: Imehaririwa:
Dakika 2
Matangazo ya kibiashara
“Khartoum imekombolewa, imekwisha,” kiongozi mkuu wa Sudani ametangaza kutoka ikulu ya rais katika hotuba iliyotangazwa kwenye televisheni ya taifa.
Katika video hii iliyorushwa na Al Jazeera, anaonekana rais wa Baraza la Utawala na kamanda mkuu wa jeshi la Sudan, Abdel Fattah Abdelrahman Burhan, akiwasili katika ikulu ya rais katika mji mkuu wa Sudani, Khartoum.
Mapema jana, jeshi la Sudani lilitangaza kuurejesha kwenye himaya yake uwanja wa ndege. Kwa mujibu wa Jenerali Nabil Abdallah, aliyewasiliana na shirika la habari la AFP, wanajeshi wa serikali “wamejilinda kikamilifu” mahali ambapo vikosi vya FSR vimekuwa wameshikilia tangu Aprili 2023.
Kilele cha mashambulizi yaliyoanza Septemba kwa siku kadhaa, wanamgambo wa Jenerali Mohamed Hamdane Daglo, anayejulikana kama Hemedti, wamekabiliwa na hali ya kushindwa baada ya kushindwa. Ijumaa ya wiki iliyopita, walitimuliwanje ya ikulu ya rais, eneo lenye ishara kubwa, na kisha kutoka vitongoji mbalimbali ambako kunapatikana Benki ya Sudani, makao makuu ya idara za kijasusi, na jumba la makumbusho la kitaifa… majengo yaliyoharibiwa na miaka miwili ya vita.
Mwanaanthropolojia Clément Deshayes anasema ni hitimisho la shambulio la bunge mnamo mwezi Septemba. “Katika siku za hivi karibuni, wakati umeongezeka kidogo tangu jeshi lilipofanikiwa kuteka tena jiji la Khartoum, ambalo lilikuwa likishikiliwa tangu mwanzo wa vita na Vikosi vya Msaada wa Haraka (RSF), na kinachotokea leo kinaonekana kuwa kukimbia kamili kwa vikosi vya RSF kutoka mji wa Khartoum,” anafafanua.
Kwa wiki kadhaa, wanajeshi wamekuwa wakiungwa mkono na wanamgambo wa kujitolea ili kuzingira maeneo ya FSR na kuwalazimisha kurudi nyuma. Kupangwa upya huku kwa jeshi kungewezesha kugeuza mzozo kulingana na Clément Deshayes. “Jeshi limeamua kufanya kile ambacho wamefanya hapo awali, yaani, jeshi lipo, lina nguvu. Lakini pamoja na vikosi, washirika, wanamgambo na vikosi mbalimbali vya wanamgambo hutumiwa kutekeleza mashambulizi. Kuna mkusanyiko mzima wa vikosi ambavyo vimeshirikiana na vinaunga mkono juhudi za vita. Hili ni jambo ambalo linatia wasiwasi sana kwa sababu kila kambi inakimbilia kuaomba msaada kwa wanamgambo,” mwanaanthropolojia anachambua.
Kulingana na jeshi la Sudani, wanamgambo hao walivuka Mto White Nile siku ya Jumatano kufika magharibi mwa nchi, hasa Darfur, eneo ambalo bado liko chini ya udhibiti wa jeshi lao kusini magharibi
Kulingana na jeshi la Sudani ngome yao ya mwisho inapatikana kusini magharibi mwa mji mkuu, eneo la kimkakati kama watafaanikiwa kurudi nyuma katika maeneo wanayodhibiti, kama vile jimbo la Darfur ambako mapigano bado yanaendelea.