Sudani: Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lalaani ukatili wa kingono dhidi ya watoto

Baada ya miaka miwili ya mzozo, Sudani sasa inakabiliwa na janga kubwa na baya zaidi la kibinadamu duniani. Hivi ndivyo Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limebainisha siku ya Alhamisi, Machi 13 huko New York. Zaidi ya watu milioni 30 watahitaji msaada wa kibinadamu, nusu yao wakiwa watoto. Wanatishiwa na njaa, mawimbi ya magonjwa ya kuambukiza ya utotoni na, hasa, na unyanyasaji wa kijinsia kutoka kwa wanamgambo.

Imechapishwa:

Dakika 1

Matangazo ya kibiashara

Na mwandishi wetu huko New York, Carrie Nooten

Mashirika mengi ya kutoa msaada wa kibinadamu yanashtumu kwamba mzozo huo unasahauliwa na kwamba jumuiya ya kimataifa imejitenga na hali hiyo.

Mkurugenzi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudunia Watoto (UNICEF)  Catherine Russell amekaririwa kwenye meza ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa alipolazimika kuorodhesha umri wa wasichana na wavulana wa Sudan waliofanyiwa ukatili wa kijinsia na watu wenye silaha, waliojifunika nyuso zao, silaha ya kisaikolojia inayozidi kutumiwa kuwatia hofu watu.

Kesi 221 za ubakaji zilirekodiwa nchini Sudan mwaka 2024, hakika mbali na jumla halisi, lakini sehemu ya waathiriwa wana umri wa chini ya miaka 5, wanne ni watoto chini ya mwaka mmoja. Katibu Mkuu wa Shirika la Madaktari Wasio na Mipaka (MSF) amekosoa tabia ya jumuiya ya kimataifa kwa kutoingilia kati hali inayoendelea nchini Sudani.

Jibu la kimataifa lisilo na maana

Vita hivi vimekuwa vikiendelea kwa karibu miaka miwili, lakini mwitikio wa kimataifa umesalia kuwa mdogo. Ahadi zilizotolewa na pande zote za kusambaza na kulinda raia zimethibitisha mara kwa mara kuwa hazifai. Mbinu za kuzingirwa, kuzuia misaada ya kibinadamu na mashambulizi ya moja kwa moja kwa raia husababisha madhara yasiyokubalika. Hii ni kweli vita dhidi ya raia, bila kujali maisha ya raia.

Kutokana na ghasia hizo, MSF ililazimika kuacha shughuli zake zote mwezi uliopita katika kambi ya watu waliokimbia makazi yao ya Zamzam, ambayo inayokumbwa na njaa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *