Sudani: Amnesty International inaishutumu China kwa kusambaza silaha kwa wanamgambo

China imetoa wito kwa raia wake kuondoka Sudani “mara moja,” hatua inayokuja baada ya kuchapishwa kwa ripoti inayoihusisha Beijing kwa kusambaza silaha kwa njia zisizo za moja kwa moja kwa wanamgambo wa Sudani. Kulingana na shirika la kimataifa la Haki za Binadamu la Amnesty International, mabomu yanayotumiwa na Vikosi vya Msaada wa Haraka (RSF) huko Darfur na Khartoum ni ya China.

Imechapishwa:

Dakika 1

Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa Amnesty International, mabomu hayo yalitambuliwa kupitia uchambuzi wa picha za vifusi vilivyopatikana baada ya mashambulizi kadhaa. Kulingana na shirika hili lisilo la kiserikali, silaha hizi ziliwasilishwa na Falme za Kiarabu kwa makundi ya kijeshi, kinyume na vikwazo vya silaha vilivyowekwa na Umoja wa Mataifa, anakumbusha Aymeric Elluin, afisaanayehusika na masuala ya utetezi katika Amnesty International.

Jambo lisilo la kawaida ni kwamba kwa mara nyingine tena, tunaona kwamba vifaa hivi havikuhamishiwa Sudani moja kwa moja, na kwa sababu nzuri, Sudani iliwekewa vikwazo, moja huko Darfur na moja kwa nchi nzima. Vifaa hivi vyote vilinunuliwa awali na Falme za Kiarabu kutoka China na kusafirishwa tena kwa Vikosi vya Msaada wa Haraka.

Falme za Kiarabu zafutilia mbali ripoti hii ya Amnesty International “Madai haya hayana msingi na hayana ushahidi,” Msaidizi wa Waziri wa Usalama na Masuala ya Kijeshi amesema katika taarifa iliyotumwa kwenye mitandao ya kijamii na Wizara ya Mambo ya Nje ya UAE.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *