Sudan yaishtaki UAE Mahakama ya ICJ kuwa imehusika na mauaji ya kimbari ya jamii ya Masalit

Mahakama ya Kimataifa ya Haki ya Umoja wa Mataifa (ICJ) imetangaza kuwa imepokea mashtaka yaliyowasilishwa na Sudan dhidi ya Muungano wa Falme za Kiarabu UAE, au Imarati ambapo Khartoum inaituhumu Abu Dhabi kuwa imekiuka Mkataba wa Mauaji ya Kimbari kwa kuwapa silaha na kuwafadhili kifedha wanamgambo wa “Vikosi vya Usaidizi wa Haraka” (RSF) katika katika vita vya ndani vya Sudan.