Sudan yaishtaki UAE kwa kuwasaidia kifedha wapiganaji wa RSF

Utawala wa kijeshi nchini Sudan, umeishtaki nchi ya Falme za Kiarabu katika mahakama ya kimataifa ya haki, ikituhumu taifa hilo la kiarabu kwa kushiriki na kuunga mkono mauaji ya halaiki yanayotekelezwa na wapiganaji wa RSF inaowasaidia.

Imechapishwa:

Matangazo ya kibiashara

Katika taarifa yake kwa vyoimbo vya habari, serikali ya Khartoum imesema imeendelea kuhoji hatua ya Umoja wa Falme za Kiarabu, atika kushiriki mauaji ya kimbari ya jumuiya ya Masalit, huko Darfur Magharibi, kupitia msaada wake wa kijeshi, kifedha na kisiasa kwa RSF.

Hata hivyo madai hayo ya Khartoum yamekanushwa vikali na UAE ikiitaja kesi hiyo kuwa ni ya kizushi na kwamba haina msingi wowote.

Tangu vita vya wenyewe kwa wenyewe vilipoanza Aprili 2023, kati ya wapiganaji wa RSF chini ya Jenerali Mohamed Hamdan Dagalo na jeshi tiifu kwa Jenerali Abdel Fattah al Burhan, pande zote zimeshutumiwa kwa kutekeleza makosa ya uhalifu wa kivita.