
Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula duniani, WFP limesema limelazimika kusitisha operesheni zake katika kubwa ya Zamzam, Kaskazini mwa Darfur nchini Sudan kwa sababu ya vita vinavyoendelea.
Imechapishwa:
Dakika 1
Matangazo ya kibiashara
WFP imesitisha utoaji wa misaada ya kuokoa maisha hasa chakula kwa maelfu ya watu waliokimbia vita kati ya jeshi na wanagambo wa RSF na kukimbilia katika kambi hiyo.
Shirika hilo linasema kwa kipindi cha wiki mbili zilizopita, machafuko yameongezeka na kulilazimu kuwahamisha wafanyakazi wake.
Laurent Bukera, ameonya kuwa iwapo vita vitaendelea na wakimbizi kutopata msaada wa chakula, katika wiki zijazo, maisha yao yatakuwa hatarini.
Aidha, ametaka pande zinazopigana kuwahakikishia usalama wafanyakazi wa WFP na wafanyakazi wa mashirika mengine yanayotoa misaada ya kibinadamu kabla ya kurejelea shughuli ya kuwasaidia wakimbizi.
Kabla ya kushuhudiwa kwa vita hivi vinavyoendelea, watu zaidi ya Milioni 1.7 walikuwa wameyakimbia makaazi yao huku wengine zaidi ya Milioni mbili wakiwa na uhitaji mkubwa wa chakula kwa mujibu wa Tume ya Umoja wa Mataifa.