Sudan: Watu 31 wameuawa katika shambulio la wapiganaji wa RSF

Watu 31, wakiwemo watoto, wameuawa na wapiganaji wa RSF katika mji Omdurman na Khartoum, kulingana na Mtandao wa Madaktari nchini Sudan.

Imechapishwa:

Dakika 1

Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa taarifa ya mtandao huo, watoto wadogo walikuwa miongoni mwa waliouawa katika kitongoji cha Al-Salha, likitaja mauaji hayo kuwa “mauaji makubwa zaidi kuwahi kurekodiwa kwenye eneo hilo”.

Katika picha za vídeo zilizosambazwa kupitia mitandao ya kijamii, zinawaonesha wapiganaji wa RSF wakiwatuhumu raia waliowakamata kuwa na uhusiano na moja ya kundi ambalo limekuwa likipigana sambamba na wanajeshi wa Serikali.

Aidha mtandao huo wa madaktari, umesema mauaji yaliyotekelezwa na wapiganaji hao ni sawa na mauaji ya halaiki, wakiitaka jumuiya ya kimataifa kuingilia kati kukomesha vita inayoendelea nchini humo.

Tangu Aprili 15, 2023, RSF imekuwa ikipambana na vikosi vya jeshi la Sudan, pande zote zikituhumiwa kutekeleza mauaji ya kiholela pamoja na vitendo vingine vya ukiukaji wa haki za binadamu.

Zaidi ya watu elfu 20 wameuawa hadi sasa, na wengine milioni 15 wamekimbia makazi yao, kulingana na ripoti za Umoja wa Mataifa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *