Sudan: Wapiganaji wa RSF watangaza kuundwa kwa serikali pinzani

Wapiganaji wa RSF nchini Sudan wametangaza kuunda serikali pinzani dhidi ya ile inyoongozwa na utawala wa kjeshi chini ya uongozi wake Jenerali Abdel Fattah al-Burhan.

Imechapishwa: Imehaririwa:

Dakika 1

Matangazo ya kibiashara

Hatua ya RSF inakuja wakati huu mapigano nchini Sudan yakiingia katika mwaka wake wa pili, mzozo ambao umepelelekea kutokea kwa mojawapo ya hali mbaya zaidi ya kibinadamu duniani.

Kulingana na kiongozi wa kundi hilo la RSF, Mohamed Hamdan “Hemedti” Dagalo, upande wake unalenga kuijenga Sudan.

Tangazo la RSF limejiri baada ya London kuwa mwenyeji wa kongamano la kujaribu kuchangisha fehda za kuisaidia nchi ya Sudan.

Abdel Fattah al-Burhan - Mkuu wa jeshi la Sudan alitangaza kulikomboa jiji hilo kutoka kwa wapiganaji wa RSF
Abdel Fattah al-Burhan – Mkuu wa jeshi la Sudan alitangaza kulikomboa jiji hilo kutoka kwa wapiganaji wa RSF via REUTERS – Sudan Transitional Sovereignty C

Mapigano yameendelea kuripotiwa kwenya taifa hilo, jeshi likisema limeshambulia kwa mabomu ngome za RSF nje ya Mji wa el-Fasher, hatua ambayo imesababisha mamia kwa maelfu ya watu kukimbilia katika kambi ya wakimbizi ya Zamzam.

Dagalo ameeleza kwamba serikali yake itatoa huduma muhimu kama elimu na afya sio tu kwa maeneo ambayo wapiganaji wake wanayakalia bali kwa raia wote wa Sudan.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *