Sudan: Wapiganaji wa RSF wamejiondoa katika mji mkuu wa Khartoum

Kiongozi wa kundi la RSF nchini Sudan, amethibitisha wapiganaji wake kujiondoa toka kwenye mji mkuu wa Khartoum, ambao kwa sasa uko chini ya udhibiti wa jeshi la Serikali.

Imechapishwa:

Dakika 1

Matangazo ya kibiashara

Tangazo la Jenerali Mohammed Hamdan Daglo, limekuja siku 3 kupita tangu kundi lake lidai kuwa halina mpango wa kuuachia mji wa Khartoum na kwamba wapiganaji wake wanajipanga upya.

Katika taarifa yake kwa vyombo vya Habari, Daglo, amekiri wapiganaji wake kuondoka Khartoum, lakini akaapa kuwa watarejea kwa nguvu bila hata hivyo kutaja ni lini watafanya hivyo.

Mapigano makali yalikuwa yakiripotiwa kati ya jeshi na wapiganaji wa RSF kuudhibiti Mji huo Mkuu.
Mapigano makali yalikuwa yakiripotiwa kati ya jeshi na wapiganaji wa RSF kuudhibiti Mji huo Mkuu. AP

Vita nchini Sudan, vimesababisha kile ambacho Umoja wa Mataifa unasema njaa mbaya zaidi duniani, watu zaidi ya milioni 12 kukosa makazi na wengine maelfu kuuawa.

Haya yakijiri kiongozi wa kijeshi jenerali Abdel Fatah al Burhan, baada ya kutangaza kuukomboa mji wa Khartoum toka kwa wapiganaji wa RSF, hapo jana alisema hakutakuwa na msamaha kwa RSF wala mazungumzo nao, huku pia akiapa kuwafurusha toka kwenye jimbo la Darfur.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *