Sudan Kusini: Wito wa kuwakutanisha rais Kiir na Makamu wake Machar watolewa

Mashirika ya kiraia nchini Sudan Kusini, yanatoa wito kwa nchi za kikanda na Jumuiya ya Kimataifa, kufanya kila kinachowezekana kuwakutanisha rais Salva Kiir na Makamu wake wa kwanza Riek Machar, ili kutatua mzozo unaofukuta.

Imechapishwa:

Dakika 1

Matangazo ya kibiashara

Sarah Nyanath kutoka shirika la Tumaini Peace Initiative aliwaongoza wenzake kuhutubia wandishi wa habari.

“Tunaelezea wasiwasi wetu juu ya kuongezeka kwa mvutano wa kisiasa, mapigano ya silaha, ghasia kati ya jamii na kuenea kwa ghasia katika maeneo kadhaa ya nchi.”

Wanaharati hawa wanasema kupata suluhisho la haraka ni lazima rais Salva Kiir na Riek Machar wakutane ana kwa ana. Hapa ni Enock Tombe, ambaye ni askofu Mstaafu.

“Kitu ambacho hawajafanya ni kuwaleta pamoja, ndio maana tunawahimiza wakuu wa nchi za IGAD waje kufanya mkutano Juba kisha wakutane”

Mwanamuziki na mwanaharakati wa haki za binadamu Manasseh Mathiang ana ujumbe kwa viongozi wa kikanda.

“Katika makubaliano ya amani, viongozi wa kikanda wamepewa jukumu kama wadhamini. Hili ni jukumu kubwa. Kama wadhamini, matarajio yetu kama raia wa Sudan Kusini ni kwamba wataongoza katika kuhakikisha kuwa pande husika zinatekeleza makubaliano ya Amani”

Wito huo unakuja wakati upande wa upinzani katika chama tawala cha SPLM unaongozwa na makamu wa rais Riek Machar kikisema kimejiondoa katika mipango ya usalama ya mkataba wa amani wa 2018 kupinga kuzuiliwa kwa viongozi wake kadhaa na kuingia kwa wanajeshi wa Uganda ndani ya Sudan Kusini.

Kenneth Lukwago, Kampala RFI Kiswahili.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *