Sudan Kusini: ‘Tuko katika hatari ya mzozo kamili katika ngazi ya taifa’

Kufuatia wito wa Rais Salva Kiir siku ya Ijumaa, Machi 7 kutakakuwataka raia kuwa na utulivu, mashirika ya kiraia nchini Sudani Kusini yanasema yana wasiwasi mkubwa kuhusu kuzuka upya kwa ghasia katika mikoa kadhaa ya nchi hiyo, hasa katika Jimbo la Upper Nile, na kukamatwa kwa viongozi kadhaa wa kisiasa.

Imechapishwa:

Dakika 1

Matangazo ya kibiashara

Akihojiwa na RFI, Jackline Nasiwa, naibu kiongozi wa Jukwaa la Mashirika ya Kiraia na mkurugenzi mtendaji wa Kituo cha Utawala Shirikishi, Amani na Haki, anabaini kwamba mchakato wa amani uko katika hatari ya kudidimia nchini Sudani Kusini na kwamba kuna hatari ya kuona nchi hiyo ikirejea katika vita vya jumla vya wenyewe kwa wenyewe.

“Nchi kwa sasa iko njia panda na ikiwa mivutano hii haitapungua, kunahatari ya nchi kutumbukia katika mzozo kamili. Watu wanarudi nyuma kwenye makabila yao, siasa zao za kikanda. Hii haitatusaidia kuponya kama serikali. Mazungumzo ya kitaifa ni muhimu sana.

“Bila jeshi la umoja, wengine hawawezi kusonga mbele vizuri”

“Pili, natoa wito wa kuunganishwa kwa jeshi. Inachukua muda mrefu sana na makundi tofauti yamehamasishwa na kujipanga upya kwa mapigano. Hivyo kunahitajika fedha nyingi na msaada kwa ajili ya kuunganisha majeshi, ili tuwe na jeshi la umoja wa kitaifa. Bila jeshi la umoja, wengine hawawezi kusonga mbele vizuri. Vyama vya siasa havitakiwi kuwa na matawi ya kijeshi. Kwa hiyo, haya yote yatatokea pale tu tunapokuwa na jeshi la taifa na wanasiasa wote wanapaswa kuchukuliwa sawa, tukiwa wanasiasa na si wanajeshi, kwa wakati mmoja,” anasema Jackline Nasiwa, naibu kiongozi wa Jukwaa la mashirika ya kiraia na Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Utawala Shirikishi, Amani na Haki.

Kwa upande wake, Tume ya Umoja wa Mataifa ya Haki za Kibinadamu nchini Sudani Kusini ina wasiwasi kuhusu “kudorora kwa hali ya kutish, hali ambayo inaweza kufuta miaka mingi ya maendeleo kuelekea amani. “

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *