
Nchini Sudani Kusini, kuna ongezeko jipya la uwezekano wa kurejea kwenye vita vya wenyewe kwa wenyewe. Makamu wa Kwanza wa Rais Riek Machar siku ya Jumatano jioni, Machi 26, amewekwa chini ya kizuizi cha nyumbani na vikosi vya usalama vya Sudan Kusini, msemaji wake ametangaza.
Imechapishwa: Imehaririwa:
Dakika 1
Matangazo ya kibiashara
Na mwanahabari wetu mjini Juba, Florence Miettaux
Mazingira kamili ya kizuizini hiki na kuhusika kwake kwa kuendelea kwa makubaliano ya amani yaliyotiwa saini mnamo 2018 hayajulikani. Umoja wa Mataifa unahofia kurejea kwa vita vya wenyewe kwa wenyewe Lakini nchi inaonekana kurudi kweye mzozo. Umoja wa Mataifa unatoa wito kwa pande husika kujizuia na kuheshimu makubaliano ya amani.
Haya ni matukio katika mzozo wa kisiasa nchini Sudani Kusini ambayo yanahofiwa kama inavyotarajiwa. Tetesi za kukamatwa kwa Riek Machar zimekuwa zikienea tangu mwanzoni mwa mwezi Machi, wakati mgogoro katika eneo la Upper Nile kaskazini mashariki mwa nchi hiyo ulisababisha kukamatwa kwa maafisa kadhaa wa chama chake mjini Juba.
Kuwekwa kwa kiongozi wa upinzani katika kifungo cha nyumbani kunatia shaka kubwa juu ya mchakato wa amani wa Sudani Kusini. Kuzuiliwa huku kunajumuisha “ukiukaji wa makubaliano ya amani” kulingana na Pal Mai Deng, msemaji wa chama cha Riek Machar. Akinukuliwa katika chombo cha habari cha ndani, ametoa wito kwa jumuiya ya kimataifa “kuhakikisha usalama wa kimwili” wa Riek Machar.
Nicholas Haysom, mkuu wa ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini, amesema katika taarifa yake. “Marekebisho ya upande mmoja ya makubaliano ya amani yanahatarisha kuirejesha nchi katika hali ya vita. “Hii sio tu itaharibu Sudani Kusini lakini eneo lote,” almesema.
Mgogoro wa sasa wa kisiasa uliongezeka wakati wanamgambo wa Nuer wanaoaminika kuwa karibu na Riek Machar waliteka kambi ya jeshi la Sudani Kusini huko Nasir mapema mwezi Machi na kumuua kamanda wake na rubani wa Umoja wa Mataifa.
Mkuu wa majeshi wa Riek Machar, pamoja na waziri wa mafuta na maafisa wengine wa chama chake, wanashutumiwa na kambi ya rais kwa kuandaa ghasia huko Upper Nile.