Sudan Kusini: Rais Kiir atangaza hali ya dharura kwenye maeneo yenye machafuko

Rais wa Sudan Kusini, Salva Kiir, ametangaza hali ya dharura kwenye majimbo yanayoshuhudia vita vya kikabila kutokana na wizi wa mifugo, ambao umesababisha maafa ya mamia ya raia.

Imechapishwa: Imehaririwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa ukurasa wa facebook wa kituo cha habari cha taifa nchini Sudan Kusini, (SSBC), Rais Salva Kiir, ametangaza hali ya dharura ya miezi sita katika majimbo ya Warrap, Mayom na jimbo la Unity, kutokana kuongezeka kwa visa vya kikabila vinavyoendelea kusababisha maafa ya raia.

Hatua ya Rais Salva Kiiri, inakuja siku chache baada yake kumteua gavana mpya wa jimbo la Warrap, ambaye amepewa jukumu la kurejesha hali ya utulivu katika jimbo hilo.

Umoja wa mataifa mapema juma hili umesema vita vya kikabila kati ya wafungaji na wakulima katika majimbo ya Tonj na Warrap vimesababisha vifo vya watu zaidi vya watu 280, tangu mwezi Machi.

Wizi wa mifugo nchini Sudan Kusini hufanyika mara kwa mara kutokana na ukame, wafugaji na wakulima wakingangania malisho ya mifugo.

Machafuko haya ya kikabila yanajiri huku taifa hilo likiendelea kushuhudia taharuki ya kisiasa katika taifa hilo changa duniani.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *