
Jeshi la Sudan Kusini, limetoa makataa ya wiki moja kwa vijana wanaomiliki silaha katika maeneo yanayoshuhudia vita vya kikabila kusalimisha silaha hizo, kabla ya oparesheni ya kuwapokea silaha kuanzishwa rasmi.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Msemaji wa Jeshi la Sudan Kusini, Lul Ruai Koang, amesema tayari kikosi maalumu kimetumwa maeneo yanashuhudia vita vya kikabila kupokea silaha hizo, iwapo juma moja litapita bila silaha kusalimishwa oparesheni maalumu ya kijeshi ya kuwapokonya vijana silaha itaendeshwa, katika majimbo ya Warrap na Mayom.
Hatua ya jeshi imekuja siku chache tu baada ya Rais Salva Kiiri, kutangaza hali ya dharura ya kipindi cha miezi sita katika majimbo hayo mawili kutokana na vita vya wakulima na wafugaji.
Mapema mwezi huu Umoja wamataifa katika ripoti yake ulisema mamia ya watu wameuawa wakiwemo 80 kwa siku za hivi karibuni kutokana vita hivyo vya kikabila.
Vita hivi vya kibalia vimetokea wakati taifa hilo linashuhudia taharuki ya kisiasa kiongozi wa upinzani Riek Machar akiwa bado anazuiliwa nyumbani.