Straika KMC amtaja Mukwala

MSHAMBULIAJI wa KMC, Daruweshi Saliboko amesema anaupenda aina ya uchezaji wa straika wa Simba, Steven Mukwala kutokana na kasi yake, mzuri wa kuunganisha pasi hadi kufunga.

Saliboko ambaye msimu huu amefunga mabao mawili na asisti moja akiwa amekosa kucheza mechi 10 kutokana na kukaa nje kwa muda mrefu akiuguza majeraha, alisema Mukwala mwanzoni alionekana hamna kitu, ila amekuja kuonyesha mabadiliko baadaye.

“Mwanzoni mwa msimu huu hakuanza vizuri maana alikuwa anakosa nafasi nyingi za kufunga, ila hakukata tamaa akajibidisha na mazoezi kwa sasa ni mshambuliaji muhimu ana mabao tisa katika ligi,” alisema Saliboko ambaye msimu uliyopita alimaliza na mabao manne na asisti tatu.

Alisema kwa upande wake hana msimu mzuri, atajitahidi kupambana kuona anaweza akaongeza bao au asisti katika mechi zilizosalia ambapo KMC itacheza dhidi ya Dodoma Jiji (Ijumaa),Simba, Tabora United,Mashujaa na Pamba.

“Japokuwa msimu huu niliumia na kukosa mechi 10 naamini panapo majaaliwa msimu unaokuja nitapambana niweze kuifikia rekodi yang ya mabao 12 niliyoyafunga nikiwa Lipuli,” alisema.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *