Spika wa Bunge la Iran: Palestina ni suala la kwanza la dunia nzima

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, kwa baraka za damu za mashahidi Palestina ni suala la kwanza la dunia nzima

Mohammad Bagher Ghalibaf, Spika wa Bunge la Jamhuri ya Kiislamu la Iran amesema hayo katika kikao cha “Mujahidina Ugenini” kilichofanyika mjini Tehran na kubainisha kwamba, suala la Palestina na mapambano dhidi ya utawala unaofanya mauaji ya kimbari wa Israel limevuka mipaka ya Iran na hata kufika katika jamii za Marekani na Ulaya.

Spika Ghalibaf amesema, kabla ya hapo Palestina ilikuwa kadhia ya kwanza ya Ulimwengu wa Kiislamu iliyokuwa ikitiliwa mkazo na sababu  ya hilo ni jukumu ambalo lilikuwa likilekezwa kwa Umma wa  Kiislamu kutokana na kuhisi kuwa ni jukumu la kidini, lakini baada ya vita vya sasa vya Gaza, Palestina haizungumziwi kama suala la Kiislamu na la kitaifa tu bali kama suala la kibinadamu.

Kwa mwaka moja sasa jeshi katili la Israel linasonga mbele na mashambulizi yake ya mara kwa mara katika Ukanda wa Gaza uliozingirwa sasa zaidi ya mwaka mmoja katika vita vya mauaji ya kimbari.

Mashambulizi ya utawala dhalimu wa Israel dhidi ya Gaza yalianza Oktoba mwaka jana, na hadi sasa utawala huo umeua karibu Wapalestina 43,000. Zaidi ya wengine 98,000 pia wamejeruhiwa tangu wakati huo.