Spika Ghalibaf: Iran inaunga mkono uthabiti nchini Sudan

Spika wa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu (Bunge la Iran), Mohammad Baqer Ghalibaf amesema Jamhuri ya Kiislamu inaunga mkono juhudi za kurejeshwa utulivu na uthabiti nchini Sudan, sanjari na kuundwa “utawala wa umoja” ambao utahakikisha kuwa taifa hilo lina mamlaka kamili ya kujitawala.