Sita wazoa bilioni ya SportPesa

Kampuni ya SportPesa imeendelea kuwaneemesha Watanzania baada ya washindi sita waliobashiri kwa usahihi mechi 13 za Mid Week Jackpot kugawana Sh 1.1 Bilioni za kampuni hiyo kwa kila mmoja kuvuna karibuni Sh 190 Milioni kwa ubashiri waliufanya.

Washindi hao walikabidhiwa mfano wa hundi za ushindi huo katika hafla iliyopfanyika juzi jijini Dar es Salaam kwa kila mmoja kuvuna Sh 188,403, 060 wanatokea mikoa tofauti ya Dar  es  Salaam, Pwani, Geita, na Lindi.

Waliovuna fedha hizo ni pamoja na Mwangwa Mwibuli (35), Mtumishi wa Umma mkazi wa Kibiti, Pwani, Frank Buchweishaija (36), Mfanyabiashara na Martin Bagule (30), mfanyakazi sekta binafsi wote wakazi wa Dar es Salaam, Colonel Moses Keyu (30), Mfanyabiashara kutoka Geita, Daud Sahani (31)- Mwalimu kutokaRuangwa Lindi na Mirambo Mswaga (29), mkazi wa Geita.

Mbali  na zawadi  kuu, washindi  watano  kati  yao walipokea  malipo  ya  ziada  kupitia muundo wa ‘double combinations’ ambao umewapa nyongeza kutokana na kuongeza nafasi za ushindi. Malipo ya ziada kwa kila mshindi ni kama ifuatavyo:  Mwangwa, Frank na Colonel kila mmoja amevuna Sh 2,850,974 kwa double combinations 128, huku Martin (2,184,444 kwa double combinations 64 na Daud (1,622,420 kwa double combinations 32.)

Mwenyekiti  wa Bodi  ya Wakurugenzi wa SportPesa, Tarimba Abbas, aliwapongeza washindi hao kwa ushindi huu mkubwa na wa kihistoria. 

“Kwa  niaba  ya Sportpesa,  ni  furaha  yangu  kubwa  sana  kuwatangaza washindi  wetu  sita  wa  Mid-week  Jackpot  ambao wameshinda jumla ya Sh1,130,423,060 ambapo kila mmoja amepokea Sh 188,403,843. Hili ni jambo la kihistoria kwa kampuni, kwani mara ya mwisho tumepata mshindi wa Mid-week Jackpot ilikuwa mwaka 2022,” alisema Tarimba.

Mmoja ya washindi hao, Mwl Daud Sahani, alisema amejisikia furaha kwa ushindi huo, kwani amecheza kwa muda mrefu kupitia magazeti na marafiki.

Mkuu wa Kitengo cha Masoko wa SportPesa, Tracy Humplick, aliwataka washindi hao kuwa mabalozi  wa  SportPesa kwa wengine. 

“Kwanza niwapongeze sana washindi wetu wa Mid-week Jackpot kwa ushindi huu mkubwa. Nyie

ni kati ya Watanzania wengi wanaopambana kimaisha na kujaribu njia tofauti za kutafuta pesa,” alisema Tracy na kuongeza; “Nawakumbusha wateja wetu wote kwamba Jackpot  bado ipo na itaendelea kuwepo. Endeleeni kubashiri na wekeni double combinations ili kuongeza nafasi za ushindi. Pia, kuna ‘Quick  Pick’.”