Njia mbili za moshi mweupe zinapoonekana kuvuka anga karibu na mstari wa mbele wa mapigano mashariki mwa Ukraine, huwa inamaanisha jambo moja: Ndege za Urusi zinakaribia kushambulia.
Lakini kilichotokea karibu na jiji la Kostyantynivka hakikuwa cha kawaida. Njia ya chini iligawanyika mara mbili na kitu kipya kikaongeza kasi kuelekea njia nyingine ya wingu hadi zilipovuka na mwangaza mkali wa rangi ya chungwa ukamulika angani.
kama wengi walivyoamini, ndege ya kivita ya Urusi iliyotungua ndege nyingine katika kile kinachoitwa shambulio hatari sana la umbali wa kilomita 20 kutoka mstari wa mbele
Ndipo Waukraine walipogundua punde kutokana na vifusi vilivyoanguka kwamba walikuwa wamejionea tu uharibifu wa silaha mpya zaidi ya Urusi – ndege isiyo na rubani ya S-70.
Hii sio droni ya kawaida. Ndege hiyo nzito isiyo na rubani inayoitwa Okhotnik (Hunter), ni kubwa kama ndege ya kivita lakini haina chumba cha marubani. Ni vigumu sana kuigundua na watengenezaji wake wanadai kuwa “haina ya kulinganishwa nayo” ulimwenguni.
Hiyo yote ni kweli, na
njia ya pili iliyoonekana kwenye video ilikuwa ni ya ndege ya Urusi ya Su-57, ikiifuata.
ndege ya Urusi .SU-57 ilikuwa ikiifuatilia S-70, na zote mbili zilikuwa zikipaa katika eneo la ulinzi wa anga la Ukraine
Ghafla S-70 ilipoteza mawasiliano na ndipo SU-57 ilipoamua kuiangamiza ili isielekee njia tofauti na lengo husika…na ndipo Waukraine walipogundua hilo….
Vita hivi vimeshuhudia ndege nyingi zisizo na rubani lakini hakuna kama S-70 ya Urusi.
Ina uzani wa zaidi ya tani 20 na inasemekana inauwezo wa masafa ya kilomita 6,000 (maili 3,700).
Ikiwa na umbo la mshale, inaonekana kuwa na umbo sawa na ya Marekani X-47B, ndege nyingine isiyo na rubani ya kivita iliyoundwa muongo mmoja uliopita.
Ndege hiyo ya Okhotnik inadaiwa kuwa na uwezo wa kubeba mabomu na roketi kwa ajili ya kupiga shabaha za ardhini na angani pamoja na kufanya uchunguzi.
Na, kwa kiasi kikubwa, imeundwa kufanya kazi kwa kushirikiana na ndege za kivita za Urusi za Su-57 za kizazi cha tano.
Imekuwa ikifanyiwa matengenezo tangu 2012 na safari ya kwanza ya ndege hiyo ilifanyika mnamo 2019.
Lakini hadi mwishoni mwa juma lililopita hakukuwa na ushahidi kwamba ilitumika katika vita vya Urusi vilivyodumu kwa miaka miwili na nusu nchini Ukraine.
Mapema mwaka huu iliripotiwa kuonekana katika uwanja wa ndege wa Akhtubinsk kusini mwa Urusi, moja ya maeneo ya uzinduzi wa mashambulizi ya Ukraine.
Kwa hivyo inawezekana kusafiri kwa ndege juu ya Kostyantynivka ilikuwa moja ya majaribio ya kwanza ya Moscow kujaribu silaha yake mpya katika hali ya mapigano.
Mabaki ya moja ya bomu la masafa marefu la D-30 la Urusi yalipatikana katika eneo la ajali ya ndege hiyo.
Je, Okhotnik inasafiri pamoja na ndege ya Su-57? . Je Rada na mifumo ya ulinzi wa Anga vilishinda kuiona SU-57 baada ya kuzimwa na S-70? HAKUNA MWENYE JIBU HADI LEO HII
JIBU WAKALITOA WARUSI WENYEWE…
Ndege hiyo isiyo na rubani inatokana na Mikoyan Skat ya awali, iliyoundwa na MiG, ikijumuisha baadhi ya teknolojia za ndege ya kivita ya Sukhoi Su-57 ya kizazi cha tano. Kufikia 2021, ilitarajiwa kufanya kazi chini ya udhibiti wa marubani wa ndege aina ya Su-57 toleo linalowezekana la siku zijazo,