
Baada ya kuibuka na ushindi mnono wa mabao 3-0 ugenini dhidi ya Tabora United, jana Jumapili, Simba imeamua kuweka kambi ya muda ya siku mbili Dodoma kabla ya kuelekea Babati siku moja kabla ya mechi yake ya Ligi Kuu dhidi ya Fountain Gate, Februari 6 katika Uwanja wa Kwaraa.
Msafara wa timu hiyo uliondoka leo asubuhi Tabora na kufika Dodoma ambako utakaa hadi kesho asubuhi Jumanne Februari 4, 2025 na kuanza safari ya Babati
Sababu mbili zimechangia Simba ifanye uamuzi huo ni kupunguza umbali wa safari ili isiwachoshe wachezaji lakini nyingine ni kukosekana kwa viwanja bora vya mazoezi Babati.
Hesabu za kwanza za Simba zilikuwa ni kuweka kambi Arusha lakini ikagundua kwamba safari ingekuwa ndefu zaidi tofauti na iwapo ikiweka kambi Babati.