
Dar es Salaam. Droo ya hatua ya 32 bora ya Kombe la Shirikisho la CRDB, imechezeshwa leo, Februari 7, 2025 huku Simba na Azam zikipangwa dhidi ya wapinzani kutoka Ligi ya Championship wakati huo mabingwa watetezi Yanga wakiangukia kwa Coastal Union.
Timu hizo tatu zote zitacheza mechi zao za hatua ya 32 bora zikiwa nyumbani na ikiwa zitasonga mbele, hatua inayofuata pia zitakuwa katika viwanja vyao vya nyumbani.
Mshindi wa mchezo baina ya Yanga na Coastal Union, katika hatua ya 16 bora atakutana na mshindi wa mchezo baina ya Polisi Tanzania na Songea United.
Katika hatua hiyo ya 32 bora, Simba ambayo imetwaa ubingw wa mashindano hayo mara tatu, itakutana na TMA Stars na itakayovuka hapo itaumana na mshindi wa mchezo kati ya Tanzania Prisons na Bigma kwenye hatua ya 16 bora.
Mabingwa mara moja wa taji hilo, Azam FC wamepangwa kucheza na Mbeya City na ikiwa watavuka.wataumana na mshindi wa mchezo baina ya Mtibwa Sugar na Towns Stars.
Ukiondoa Yanga na Coastal Union, timu nyingine za Ligi Kuu ambazo zitakutana zenyewe ni Kagera Sugar na Namungo.
Ukiondoa mechi hizo, nyingine ni baina ya Tabora United dhidi ya Transit Camp, Mashujaa na Geita Gold, Fountain Gate itaumana na Stand United huku Singida Black Stars ikipangwa kukabiliana na Leo Tena.
Kuna mechi ya JKT Tanzania na Biashara United, Kiluvya United na Pamba Jiji, Girrafe Academy dhidi ya Green Warriors, Cosmopolitan itacheza na KMC na Mbeya Kwanza itaikabili Mambali Academy.
RATIBA KAMILI
Cosmopolitan FC vs KMC FC
Mbeya Kwanza vs Mambali Academy
Tanzania Prisons vs Big Man
Kagera Sugar vs Namungo
Polisi Tanzania vs Songea United
Kiluvya Utd vs Pamba Jiji FC
Mtibwa Sugar vs Towns Stars
Giraffe Academy vs Green Warriors
JKT Tanzania vs Biashara Utd
Tabora Utd vs Transit Camp
Mashujaa FC vs Geita Gold
Simba SC vs TMA Stars
Azam FC vs Mbeya City
Singida BS vs Leo Tena
Yanga SC vs Coastal Union
Fountain Gate vs Stand Utd