Simba yamganda kiungo Sfaxien

MABOSI wa Simba wamemganda kiungo wa CS Sfaxien ya Tunisia, Balla Moussa Conte baada ya kufanya naye mazungumzo na sasa wanasikilizia uamuzi wa mwisho wa klabu anayoichezea ili atue Msimbazi msimu ujao.

Simba ilimuona kiungo huyo katika mechi ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika ilipoichapa CS Sfaxien Kwa Mkapa kwa mabao 2-1 kisha kwenda kuifunga kwake  1-0.

Hata hivyo Mwanaspoti linafahamu dili hilo liliishia njiani katika dirisha dogo licha ya mazungumzo ya mwisho mchezaji huyo kuwaambia wampe pesa ili asitishe mkataba alionao kwa Waarabu hao.

Taarifa za ndani zinasema Simba ilikubaliana na Conte mwishoni mwa msimu kwamba itampatia pesa ambazo wamekubaliana ili auze mkataba wake na hivi karibuni ilirudi kukumbushia.

“Ili kiungo huyo atue ndani ya Simba inabidi amalize mkataba a

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *