Simba Queens yaanza na straika

MABINGWA watetezi wa Ligi Kuu ya Wanawake, Simba Queens wameanza kumfuatilia mshambuliaji wa CBE na timu ya taifa ya Ethiopia, Senaf Wakuma.

Inaelezwa timu hiyo wakati wa usajili itapitisha fagio kwa wachezaji takribani saba ikiwemo eneo la ushambuliaji ili kusajili nyota wapya.

Hata hivyo, kocha wa timu hiyo, Yussif Basigi inaelezwa pia hatakuwa sehemu ya kikosi hicho msimu ujao kutokana na kushindwa kuonyesha kiwango kizuri msimu huu.

Eneo la beki wa kati, kipa na kiungo ni miongoni mwa maboresho watakayoyafanya Simba msimu ujao sasa imeanza mazungumzo na Wakuma kuwa nae msimu ujao.

Chanzo kiliambia Mwanaspoti kuwa kinachosubiriwa kwa sasa ni majibu ya mchezaji lakini viongozi wanatamani kuwa nae msimu ujao kutokana na kiwango bora alichoonyesha kwenye misimu miwili ya ligi hiyo.

“Hiyo ni ripoti ya kocha Basigi alisema anahitaji mshambuliaji mwingine wa kati nje ya Shikangwa hivyo viongozi wanafuatilia kwa ukaribu na klabu yake lakini inavyoonekana ugumu upo kwa mchezaji ,” kilisema chanzo hiko.

Mshambuliaji huyo amemaliza kinara wa ufungaji kwenye ligi hiyo akifunga  mabao 20 jumla, ndani ya misimu miwili ya ligi kuu amefunga mabao 48 katika mechi 46.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *