Sillah bado kiduchu atimize ndoto

MSHAMBULIAJI wa Azam FC, Gibril Sillah ameendelea kuisogelea ndoto yake ya kumaliza na mabao kuanzia 10  msimu huu, huku akiamini mechi sita zilizosalia atalitimiza hilo.

Azam FC imecheza mechi 24 ikishinda 15, sare sita, imefungwa michezo mitatu ikimiliki mabao 38, imefungwa 12 ikiwa na pointi 51, jambo ambalo Sillah anaamini njia ya kufikia malengo yake ipo wazi.

Sillah amefikia rekodi yake ya mabao manane aliyoyafunga msimu uliopita katika mechi dhidi ya  Yanga 3-2, (Oktoba 2023, (Azam 2-1 Yanga, Machi 13), (Azam 5-0 KMC, Desemba 7, 2023), (KMC 0-4 Azam, Septemba 19) na timu nyingine alizozifunga ni Geita Gold, Mashujaa na Mtibwa Sugar.

“Nimeifikia rekodi yangu ya mabao manane ya msimu uliopita. Ndiyo maana naona mechi zilizosalia naweza nikatimiza ndoto yangu ya kufunga mabao kuanzia 10 na kuendelea na hilo linawezekana kikubwa ni kuomba afya njema,” alisema na kuongeza:

“Ligi ilipofikia ni ngumu, kila timu inakwenda kutimiza malengo yake, lakini nitapambana kwa kadri niwezavyo ili kutimiza malengo yangu na ya timu kiujumla .”

Sillah alisema kitu alichokipenda msimu huu ni ushindani ambao unamfanya asibweteke na unamsaidia kucheza kwa kiwango cha juu, kuhakikisha anaisaidia timu yake kwa muda anaokuwepo uwanjani.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *