
Theluthi mbili ya misaada ya Marekani ilikuwa ikitolewa kwa nchi za Afrika, kufadhili barabara, umeme na umwagiliaji. Kujiondoa kwa Washington kunaacha miradi ambayo haijakamilika na kudhoofisha uchumi wa nchi hizi.
Imechapishwa:
Dakika 2
Matangazo ya kibiashara
Hali hiyo imeansa kujitokeza nchini Côte d’Ivoire. Wafanyakazi bado wana shughuli nyingi kwenye makutano makubwa ya Koumassi mjini Abidjan. Miundombinu inayofadhiliwa na shirika la maendele la Marekani la MCC “Millennium Challenge Corporation” chini ya mpango wa Côte d’Ivoire: dola milioni 537 kwa jumla. Hasa kwa ajili ya ukarabati wa barabara kuu ya Boulevard du Port. Mradi huo ni wa miaka mingi, lakini ni ufadhili wa Marekani ambao ulifanikisha hili, anaelezea Marie-Viviane Ado Gossan-Coulibaly, mkurugenzi wa MCA Côte d’Ivoire, chombo kinachohusika na kutekeleza programu. “Ni njia muhimu katika uchumi wa Côte d’Ivoire kwa sababu bidhaa zote hupitia njia hii kuuzwa nje ya nchi au hata kuagizwa nje. Pia, viwanda vingi viko katika eneo hilo, kiwada cha kutengeeza saruji, kiwanda cha kahawa, kiwanda cha kakao. Na ukarabati wa barabara kama hiyo una athari kubwa katika utendaji wa tasnia hizi zote.”
Malawi yanyimwa ufadhili wa barabara zake
Nchini Malawi, ufadhili wa dola milioni 350 unatoweka. Ulikuwa utumike kwa ujenzi wa barabara nchini kote. Jacob Hara, Waziri wa Uchukuzi, amethibitisha hili: mradi uliahirishwa baada ya, amesema, “mabadiliko ya ghafla katika sera ya Marekani.” “Fundisho jipya la kuhalalisha matumizi ya umma kimataifa limegusa tena. Kwa Ibrahim Amadou Louché, mwanauchumi wa Niger, matokeo yanapita nje ya mipaka ya Afrika: “Hatari ni kwamba itazidisha matatizo ambayo tayari yapo sana katika maeneo haya ambayo, kwa ricochet, huishia kufikia nchi zilizoendelea kupitia njia mbalimbali, hasa kwa njia ya uhamiaji au mwenyeji. Ingefaa kwa mamlaka ya Marekani kufikiria upya msimamo wakeo na kujaribu kurejesha msaada huu. »
“Mtazamo mbaya”
Marekani imsitisha miradi ya USAID, Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo ya Kimataifa: dola bilioni 16 katika msaada wa kila mwaka kwa Kusini mwa Jangwa la Sahara. Ufaransa na Uingereza pia zimepunguza misaada yao ya maendeleo. Hii inaanza kufikia ufadhili mwingi ambao mataifa ya Afrika yatakosa. “Kuna chuki. Mashirika ya kimataifa pia yanaajiri wafanyakazi wa ndani. Kuna kazi za moja kwa moja na zisizo za moja kwa moja, anasema Ibrahim Amadou Louche. Binafsi, nina marafiki ambao sasa wanajiandaa kurejea nchini, na kwa kweli kuna maswali mengi kuhusu mustakabali wao. Mtazamo unazidi kuwa mbaya.”
Njia mbadala ya nchi hizi itakuwa kugeukia zaidi Uchina kwa ufadhili. Lakini Beijing iko kwenye mtindo tofauti, unaotegemea uwekezaji na wenzao. Ambayo inachangia madeni ya nchi. Kilio cha mbali kabisa na michango ya MCC ya kutorejesha pesa.