Shura ya Maimamu Tanzania yakaribisha kuachiwa huru Masheikh 12

Shura ya Maimamu Tanzania imepokea kwa mikono miwili uamuzi wa mahakama wa kuwaachia huru Masheikh 12 waliokaa gerezani miaka 10, (2015-2025), kwa tuhuma za ugaidi. Uamuzi huo umetolewa na Jaji wa Mahakama Kuu Mheshimiwa Arnold John Kirekiano.