Shirika la Ujasusi la Russia: NATO inapanga kumuondoa madarakani rais wa Ukraine, Zelensky

Shirika la kijeshi la NATO linafikiria kufanikisha mpango wa kumuondoa madarakani Rais wa Ukraine Vladimir Zelensky kwa ‘kumchafua’ kabla ya uchaguzi ujao utakaofanyika mwakani. Hayo yameelezwa katika ripoti iliyotolewa na Shirika la Ujasusi la Russia la Nje ya Nchi (SVR).