Shirika la ndege la Kenya laanza tena kurekodi faida baada ya miaka 10

Baada ya kipindi cha zaidi ya miaka 10 cha msukosuko wa kifedha, shirika la ndege la Kenya, limeanza tena kuripoti faida.

Imechapishwa:

Dakika 1

Matangazo ya kibiashara

Tangu mwaka wa 2012, shirika hilo la ndege halijawa likiandikisha faida ambapo sasa wachambuzi wa masuala ya uchumi wanasema limeanza kuandikisha faida kutokana na mageuzi kadhaa yanayoendelea kutekelezwa.

Kenya Airways, mojawapo ya mashirika makubwa zaidi ya ndege barani Afrika, imeripoti kuongezeka kwa uuzaji wa tiketi za kusafiria kwa wateja wake.

Shirika hilo limeonekana kuimarisha safari zake za ndege za kwenda London na Marekani suala ambalo wachambuzi wanasema huenda pia limechangia kuimarika kwake.

Kenya Airways pia imebadilisha ndege zake za zamani na zile za kisasa ambazo zinarahisisha usafiri wake.

Kenya Airways, mojawapo ya mashirika makubwa zaidi ya ndege barani Afrika, imeripoti kuongezeka kwa uuzaji wa tiketi za kusafiria kwa wateja wake.
Kenya Airways, mojawapo ya mashirika makubwa zaidi ya ndege barani Afrika, imeripoti kuongezeka kwa uuzaji wa tiketi za kusafiria kwa wateja wake. © REUTERS/Monicah Mwangi

Kuimarika kwa shillingi ya kenya dhdii ya Dolla ya Marekani mwaka uliopita pia imechangia katika ukuwaji wa shirika hilo.

Serikali ya Kenya ambayo mara kwa mara ilikuwa ikilisaidia shirika hilo kifedha kuendelea na shughuli zake, imekuwa pia ikitafuta mwekezaji wa kibinafsi hadi sasa haijaweza kufanikisha hilo.

Mashirika ya ndege kama vile American Airline yamekuwa yakihusishwa na mpango wa kuwekeza kwenye shirika hilo.

Mkurugenzi Mtendaji wa shirika hilo sasa ameweka rekodi ya idadi kubwa zaidi ya abiria wanaobebwa na mapato haya yanaonesha uwezo wa kampuni hiyo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *