Shinyanga ligi ni Mei Mosi

Ligi ya Kikapu Mkoa wa Shinyanga  imepangwa kuanza Mei 1 na kinachosubiriwa kwa sasa ni timu kuthibitisha kwa kulipia fomu za ushiriki.

Kamishina wa ufundi na mashindano wa mkoa huo, George Simba alizitaja timu zitakazoshiriki ni Risasi, Kambarage Warriors, B4 Mwadui, Kahama Sixers, na Veta Shinyanga.

Alisema timu  itakayolipa Sh100,000 ndiyo itakayooshiriki mashindano hayo.

“Ligi haiwezi ikafanyika hadi klabu zilizothibitisha kushiriki mashindano hayo zilipe ada hiyo,” alisema Simba, huku akizitaka timu zote ziendee na mazoezi.

Katika fainali ya mwaka jana, Kahama Sixers iliifunga Risasi kwa pointi 67-62, katika Uwanja wa Risasi na zilicheza michezo mitatu ‘best of three pray off’, na Sixers kushinda  michezo 2-1.

Katika mchezo wa kwanza, Risasi ilishinda  kwa pointi 102-100, huku Kahama Sixers ikishinda michezo miwili kwa pointi 87-60 na 67-62.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *