Shida ya Spurs iko hapa

London, England.  Miaka 17 imepita sasa tangu Tottenham Hotspur mara ya mwisho ilipoonja utamu wa kushinda ubingwa, iliponyakua Kombe la Ligi.

Na wakati makocha wa mataji Antonio Conte na Jose Mourinho wakipita kwenye klabu hiyo na kutoka patupu bila ya taji lolote, kumekuwa na kawaida ya wachezaji wa Spurs kwenda kushinda mataji huko kwingine baada ya kuachana na miamba hiyo ya London kaskazini.

Beki wa pembeni Kieran Trippier alinyakua taji lake la pili tangu alipoachana na Spurs baada ya kuisaidia Newcastle United kubeba Kombe la Ligi kwa kuichapa Liverpool, Jumapili iliyopita.

Gundu la kubeba mataji kwa Spurs na mastaa wake, limebaki kwa straika Harry Kane pekee, baada ya kushuhudia wachezaji 44 walioachana na timu hiyo wote kwenda kubeba mataji kwingineko.

Na kwa Kane, matumaini anaweza kumaliza gundu hilo mwishoni mwa msimu huu baada ya Bayern Munich kuongoza msimamo wa Bundesliga kwa tofauti ya pointi sita dhidi ya Bayer Leverkusen.

Na mataji hayo yaliyobebwa na wachezaji wa Spurs hayahusu wale waliokwenda kubeba ubingwa wakiwa kwa mkopo kwenye timu nyingine, Bryan Gil na Giovani Lo Celso.

Mastaa hao walibeba mataji baada ya kuondoka Spurs, ambayo taji lake la mwisho lilikuwa 2008.

1. Luka Modric; Amebeba La Liga mara nne, Ligi ya Mabingwa Ulaya mara sita Real Madrid.

2. Kyle Walker; Amebeba mataji sita ya Ligi Kuu England akiwa na Manchester City

3. Kieran Trippier; Amebeba La Liga akiwa Atletico Madrid na Kombe la Ligi na Newcastle.

4. Lucas Moura; Amebeba mataji matatu tangu alirudi Sao Paulo, Brazil.

5. Toby Alderweireld; Ameshinda mataji mawili akiwa Royal Antwerp

6. Jan Vertonghen; Ameshinda ubingwa wa Ligi Kuu Ureno akiwa Benfica

7. Christian Eriksen; Ameshinda Kombe la FA na Kombe la Ligi akiwa Manchester United.

8. Davinson Sanchez; Ameshinda Super Lig akiwa Galatasaray ya Uturuki

9. Tanguy Ndombele; Ameshinda Super Lig akiwa Galatasaray

10. Carlos Vinicius; Ameshinda Super Lig akiwa na Galatasaray

11. Erik Lamela; Ameshinda Europa League akiwa Sevilla

12. Etienne Capoue; Ameshinda Europa League akiwa Villarreal

13. Juan Foyth; Ameshinda Europa League akiwa Villarreal.

14. Roman Pavlyuchenko; Ameshinda ubingwa akiwa Lokomotiv Moscow ya Russia

15. Vedran Corluka; Ameshinda ubingwa wa ligi na makombe ya ndani akiwa Lokomotiv Moscow

16. Rafael van der Vaart; Ameshinda Superliga akiwa FC Midtjylland ya Denmark.

17. Joe Hart; Amebeba mataji saba akiwa Celtic.

18. Cameron Carter-Vickers; Ameshinda mataji akiwa Celtic chini ya Ange Postecoglou

19. DeAndre Yedlin; Ameshinda Championship akiwa Newcastle na Kombe la Ligi akiwa Inter Miami.

20. Paulinho; Ameshinda mataji Barcelona na akiwa Guangzhou Evergrande ya China.

21. Harry Winks; Alishinda Championship akiwa Leicester City

22. Georges-Kevin Nkoudou; Ameshinda ubingwa wa Uturuki akiwa Besiktas.

23. Fernando Llorente; Ameshinda Coppa Italia akiwa Napoli

24. Vincent Janssen; Amebeba ubingwa wa ligi akiwa Monterrey na Royal Antwerp

25. Paulo Gazzaniga; Amebeba Championship akiwa Fulham.

26. Josh Onomah; Alishinda Championship akiwa Fulham

27. Benjamin Stambouli; Ameshinda ubingwa wa Ligue 1 akiwa PSG.

28. Kevin Prince-Boateng; Amebeba mataji AC Milan, Eintracht Frankfurt na Barcelona.

29. Clint Dempsey; Amebeba mataji akiwa Seattle Sounders.

30. Steven Pienaar; Ameshinda ubingwa akiwa Afrika Kusini

31. Vlad Chiriches; Amebeba mataji ya ligi mara tatu huko Romania akiwa FCSB.

32. Pierluigi Gollini; Ameshindwa Serie A akiwa Napoli.

33. Adam Smith; Ameshinda Championship akiwa Bournemouth.

34. Zeki Fryers; Amebeba League Two akiwa Swindon Town.

35. Fraizer Campbell; Ameshinda Championship akiwa Cardiff.

36. Jimmy Walker; Ameshinda National League akiwa Lincoln kabla hajastafu.

37. Hossam Ghaly; Ameshinda Ligi ya Mabingwa Afrika akiwa na Al Ahly.

38. Paul-Jose M’Poku; Ameshinda Kombe la Ubelgiji akiwa Standard Liege.

39. Tomislav Gomelt; Ameshinda Kombe la Romania akiwa CFR Cluj.

40. Simon Dawkins; Ameshinda taji akiwa San Jose Earthquakes ya MLS.

41. Tomas Pekhart; Ameshinda ubingwa wa ligi AEK Athens, Hapoel Be’er Sheva na Legia Warsaw.

42. Bongani Khumalo; Ameshinda mataji ya kutosha akiwa kwao Afrika Kusini

43. Nathan Oduwa; Ameshindwa ubingwa wa ligi na makombe akiwa Olimpija Ljubljana.

44. Tom Glover; Amebeba mataji matatu akiwa na Melbourne City.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *