Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta amesaini jana sheria inayo ruhusu mwanaume kuoa wake kulingana na idadi anaohitaji, bila hata hivo kumfahamisha mke wake au wake zake, imethibitisha ikulu ya rais
Imechapishwa:
Matangazo ya kibiashara
Baraza la Kitaifa la kanisa nchini Kenya (NCCK), ambalo linajumuisha zaidi ya madhehebu na mashirika ya kikristo 40, limepinga sheria hio, huku shirikisho la kitaifa la mawakili likibaini kwamba litakata rufaa ili sheria hio ifutwe.
Tabia ya kuoa wake zaidi ya mmoja imesambaa nchini Kenya, hususan katika maeneo ya vijijini na katika jamii ya waislamu nchini Kenya. Kulingana takwimu za hivi karibuni, katika mwaka wa 2009, asilimia 13 ya wanawake wa Kenya walibanini kwamba wanaishi katika ujumba wa mwanaume kuwa na wanawake zaidi ya mmoja.
“Wakati unamuoa mwanamke wa kiafrika, anapaswa kufahamu kwamba, mwanake wa pili yuko njiani, na wa tatu (…), hii ni Afrika”, amesema Junet Mohamed, katika mdahalo uliyokua umeandaliwa kuhusu suala hilo.

Wakati huo huo Muungano wa Maendeleo ya wanawake nchini Kenya unapanga kumwomba rais wa nchi hiyo Uhuru Kenyatta kubadilisha sheria aliyotia saini jana inayowapa wanaume nchini humo, kuoa wanawake zaidi ya mmoja mbali na wale dini ya Kislamu.
Muungano huo umeungwa mkono pia na vioongozi wa dini ya Kikristo nchini humo ambao wamepinga sheria hiyo mpya iliyopitishwa na bunge la Kenya mapema mwaka huu.
Sheria hii inamruhusu mwanaume nchini Kenya kuoa wake wengi anavyopenda bila ya kumfahamisha mke wa kwanza.