Sheikh Naim Qassem: Maziko rasmi ya Shahidi Hassan Nasrullah yatafanyika Lebanon Februari 23

Mazishi ya kiongozi wa muda mrefu wa Harakati ya Hizbullah ya Lebanon Sayyid Hassan Nasrullah yatafanyika Februari 23, miezi kadhaa tangu alipouawa shahidi katika shambulio la kigaidi la anga lililofanywa na jeshi la utawala wa Kizayuni wa Israel katika mji mkuu wa Lebanon, Beirut.