
Khatibu wa Swala ya Ijumaa iliyosaliwa leo hapa mjini Tehran amesema kuhusu mashambulizi ya hivi karibuni ya utawala wa Kizayuni dhidi ya Iran kwamba, haki ya kujibu uchokozi huo imehifadhiwa kwa mujibu wa Kifungu cha 51 cha Mkataba wa Umoja wa Mataifa.
Hujjatul Islam wal Muslimin Sheikh Kadhim Siddiqi amesema hayo leo mbele ya hadhara kubwa ya waumini waliohudhuria ibada ya Sala ya Ijumaa hapa Tehran na kueleza kwamba hujuma ya genge la kigaidi la utawala wa Kizayuni dhidi ya Iran yenye nguvu ambayo ni chimbuko la wanaume wote shupavu, ni ishara ya upumbavu na fikra fupi za utawala huo ghasibu.
Ayatullah Siddiqi amesisitiza kuwa, Iran ina haki kamili ya kujibu uchokozi huo na haki hiyo imehifadhiwa kwa mujibu wa Kifungu cha 51 cha Mkataba wa Umoja wa Mataifa.
Khatibuu wa muda wa Sala ya Ijumaa Tehran amesema, utawala wa Kizayuni ulidhani kuwa, iwapo utaivamia Iran, wananchi wangeacha mambo yao na kwenda kwenye maficho sawa na viongozi wao waoga.
Kadhalika ameeleza kuwa, Wazayuni walikosea mahesabu kuhusiana na Iran kwani hadi sasa bado hawajafahamu uwezo, nguvu, ubunifu na azma ya taifa la Iran, hivyo sisi tunapaswa kutoa somo la hilo.