
Siku moja baada ya shambulio la kombora la balestiki la Urusi katikati mwa jiji la Sumy, nchini Ukraine ambalo limesababisha vifo vya watu 34 na zaidi ya 100 kujeruhiwa, idadi ya watu imeshtuka. Kyiv inaonya kuwa Urusi haina nia ya kusitisha mashambulizi yake, wakati Moscow imelisema siku ya Jumatatu kuwa imelenga mkutano mkuu wa wafanyaikazi.
Imechapishwa:
Dakika 1
Matangazo ya kibiashara
Urusi imetangaza Jumatatu kwamba imeshambulia mkutano wa kijeshi wa Ukraine huko Sumy siku iliyopita kwa makombora ya balestiki, huku ikiituhumu Kyiv kuwatumia raia kama “ngao za binadamu.”
Wizara ya Ulinzi ya Urusi imesema katika taarifa kwamba wanajeshi wake wametumia makombora mawili ya balistiki ya Iskander kwenye “mahali pa mkutano wa maamuzi” ya kundi la jeshi la Ukraine huko Sumy. Ukraine “inaendelea kutumia raia wake kama ngao ya binadamu, kwa kuweka vituo vya kijeshi au kuandaa matukio yanayohusisha wanajeshi katikati mwa jiji lenye watu wengi,” wizara ya Urusi imeongeza.
Maombolezo nchini Ukraine
Picha za eneo la katikati mwa jiji lililoharibiwa la Sumy zinaendelea kushtua Ukraine, ambapo mikoa kadhaa imetangaza siku ya maombolezo kwa wahasiriwa wa shambulio la Jumapili kwenye eneo la mijini lenye shughuli nyingi, anakumbusha mwandishi wetu huko Kyiv, Emmanuelle Chaze.
Miongoni mwa wahasiriwa walikuwa watoto wawili na mwanamuziki kutoka Sumy Symphony Opera. Vifo hivi ni ukumbusho kwamba raia ndio wa kwanza kuteseka kutokana na mashambulizi haya kwenye maeneo yenye watu wengi.
Mashambulizi haya ya mara kwa mara, tangu shambulio hili la Sumy unakuja wiki moja tu baada ya vifo vya watu 20 huko Kryvyi Rih, ambayo amekatisha tamaa raia. Pia kuna hali ya kutojiweza katika kukabiliana na miashambulizi kama hiyo, hivyo basi wito wa kyiv wa mara kwa mara kwa washirika wa Ukraine kutafuta rasilimali zaidi za kujilinda dhidi ya mashambulizi haya ya anga.
Idara ya ujasusi ya Ukraine imetangaza kuwa imetambua brigedi za Urusi ambazo zilizindua mashambulizi haya. Pia ni njia ya Ukraine kuonyesha ulimwengu mzima kwamba Kyiv inakusudia kujibu, haswa kisheria, kwa mashambulio kama haya, kwani ndege zisizo na rubani za Urusi ziliendelea kuanguka huko Ukraine jana usiku. Miji ya Odessa, Kharkiv na Zaporizhzhia imeashambuliwa.