
Dar es Salaam. Serikali imetangaza nafasi 15 za ajira mpya katika kada za ujenzi na mifugo, ambapo mwisho wa kutuma maombi ni Februari 28, 2025.
Tangazo la nafasi hizo limetolewa jana Februari 19, 2025 na Katibu wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma huku akiwataka wenye sifa kuomba kupitia akaunti zao za Ajira Portal.
“Katibu wa Sekretarieti ya Ajira Katika Utumishi wa Umma, kwa niaba ya Wizara, Idara zinazojitegemea, Wakala za Serikali, Tawala za Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa (MDAs & LGAs) anakaribisha maombi ya kazi kutoka kwa Watanzania wenye sifa na uwezo wa kujaza nafasi kumi na tano (15) kama ilivyoainishwa katika tangazo hili,” limeeleza tangazo hilo.
Nafasi zinazotakiwa kujazwa ni pamoja na: Mkadiriaji Majenzi Daraja la II (Quantity Surveyor II) – nafasi 5, Ofisa Mifugo Daraja la II (Livestock Officer II) – nafasi 5 na Ofisa Mifugo Msaidizi Daraja la II (Livestock Field Officer II) – nafasi 5.