SERIKALI YAONGEZA UDAHILI WANAFUNZI WA AFYA
#HABARI: Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeongeza udahili wa wanafunzi wa Taaluma za Afya ngazi ya kati, kutoka wanafunzi 20,030 mwaka 2020 hadi kufikia wanafunzi 25,390, ili kuounguza changamoto za upatikanaji wa watumishi wa kada hiyo.
Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu, amesema hayo wakati akitaja maazimio ya mkutano wa Siku Tatu wa rasilimali watu, ulioandaliwa na Taasisi ya Hayati Benjamini Mkapa, ikiwa ni kumbukizi ya alioyafanya katika Sekta ya Afya, kwenye Ukimbi wa Mikutano wa Kimataifa Julius Nyerere (JNICC) Jijini Dar aes Salaam.
“Wanafunzi waliodahiliwa katika vyuo vikuu ngazi ya Shahada walikuwa elfu 5,674 mwaka 2023, ikilinganishwa na wanafunzi elfu 4,324 Mwaka 2020, hii itasaidia kupunguza changamoto ya upungufu wa watumishi inayopelekea wananchi kupata huduma kwa wakati.” Waziri Ummy.