Serikali ya Uingereza imetoa zaidi ya shilingi bilioni tatu kwa Shirika la Umeme nchini (TANESCO) kuwezesha programu ya kuhamasi…

Serikali ya Uingereza imetoa zaidi ya shilingi bilioni tatu kwa Shirika la Umeme nchini (TANESCO) kuwezesha programu ya kuhamasi…

Serikali ya Uingereza imetoa zaidi ya shilingi bilioni tatu kwa Shirika la Umeme nchini (TANESCO) kuwezesha programu ya kuhamasisha matumizi ya teknolojia ya majiko ya umeme katika kupikia, ili kufikia lengo la asilimia 80 ya Watanzania wanaotumia nishati safi ya kupikia ifikapo mwaka 2034.

Akizungumza jijini Dar es Salaam wakati wa uzinduzi wa programu ya ‘Pika Smart’ ambayo imelenga kuongeza hamasa ya matumizi ya teknolojia ya umeme katika kupikia, Kamishna wa Nishati Jadidifu kutoka Wizara ya Nishati, Mhandisi Innocent Luoga, amesema programu hiyo inaendana na mkakati wa serikali wa kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia.

#AzamTVUpdates
Mhariri | John Mbalamwezi

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *