Serikali ya Poland yashinda kura ya imani

Serikali hiyo imeshinda kura hiyo kwa kura 243 dhidi ya 210.

Kura hiyo iliitwa na Waziri Mkuu Donald Tusk baada ya mzalendo Karol Nawrocki kushinda urais, na kuwapelekea wataalam kutabiri kuwa serikali itadhoofishwa na kupelekea uchaguzi wa mapema.

“Naitisha kura ya imani kwa kuwa nina imani kwamba tuna mamlaka ya kuongoza,” alisema Tusk mwanzoni mwa kikao cha bunge cha Jumatano.

Nawrocki ambaye ni shabiki wa Rais wa Marekani Donald Trump, anatarajiwa kujaribu kuiangusha serikali na kukiongezea umaarufu chama kilichomuunga mkono cha Sheria na Haki, PiS.

Tusk, ambaye ni rais wa zamani wa Umoja wa Ulaya, aliingia mamlakani mwaka 2023 kama mkuu wa muungano wa chama chake cha mrengo wa kati Polish People’s Party, PSL na chama cha mrengo wa kushoto cha New Left.

Hakujapangwa uchaguzi mpya wa bunge hadi mwaka 2027 nchini Poland.

Tusk alitarajiwa kushinda kura hiyo kwa kuwa muungano wake una wingi wa viti 242 kati ya viti 460 bungeni na anahitaji wingi mdogo tu kushinda.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *