Serikali ya Gaza: Zaidi ya Wapalestina elfu 61 wameuawa shahidi, familia 2,092 zimefutwa kabisa

Idara ya Vyombo vya Habari ya Serikali huko Gaza imesema kuwa vita vya maangamizi vilivyoanzishwa na utawala ghasibu wa Israel katika Ukanda wa Gaza vimeua shahidi zaidi ya Wapalestina 61,000, na kuwalazimisha wengine zaidi ya milioni mbili kuwa wakimbizi, na kwamba baadhi yao walilazimika kukimbia zaidi ya mara 25, katika maafa ambao hayajawahi kutokea katika historia.