Serikali imetangaza matokeo ya utafiti wa kitaifa wa mwaka 2024 kuhusu ukatili dhidi ya watoto na vijana, yakionesha kupungua kwa matukio ya ukatili ikilinganishwa na miaka ya nyuma.
Akizungumza wakati wa kuwasilisha ripoti hiyo, Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalumu, Dkt. Dorothy Gwajima amesema japokuwa matukio yamepungua bado machache yanaendelea kutokea na kuwaathiri watoto na vijana hususan katika eneo la afya ya akili.
Utafiti huo umehusisha watoto zaidi ya 11,000 katika mikoa 31 ya Tanzania, ukilenga kutoa picha halisi ya hali ya ukatili nchini na kusaidia mikakati ya kuwalinda watoto.
#azamnewsupdates
✍Upendo Michael
Mhariri| @official_jennifersumi