Serikali imesema itahakikisha chakula kinachozalishwa na kuuzwa nchini ni salama kwa afya ya mlaji, na kwamba itachukua hatua ka…

Serikali imesema itahakikisha chakula kinachozalishwa na kuuzwa nchini ni salama kwa afya ya mlaji, na kwamba itachukua hatua ka…

Serikali imesema itahakikisha chakula kinachozalishwa na kuuzwa nchini ni salama kwa afya ya mlaji, na kwamba itachukua hatua kali dhidi ya yeyote atakayevuruga usalama wa chakula.

Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Exaud Kigahe amesema hayo jijini Dar es Salaam katika maadhimisho ya siku ya chakula salama duniani. Amesema kuwa ili kufanikisha hilo, tayari Shirika la Viwango Tanzania (TBS) limeandaa mpango wa kitaifa wa kukabiliana na dharura za usalama wa chakula, kwa lengo la kulinda afya ya wananchi na kuimarisha mifumo ya chakula nchini.

#AzamTVUpdates
✍Juliana James
Mhariri | John Mbalamwezi

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *