Serikali imepanga kuweka unafuu wa kodi ya mapato kwa vyombo vidogo vya usafirishaji ikiwemo pikipiki za miguu miwili (bodaboda), miguu mitatu (bajaji) na magari ya mizigo yenye uzito usiozidi kilo 500 (kama Guta), kwa kupitia maboresho ya viwango vya kodi elekezi.
“Kwa mujibu wa Jedwali Na. 1 la mapendekezo ya bajeti, utaratibu mpya wa ukadiriaji kodi utaruhusu kundi hili kutekeleza sheria kwa urahisi huku wakipunguziwa mzigo wa kodi.” amesema, Waziri wa Fedha, Dkt. Mwigulu Nchemba.
Dkt. Mwigulu amesema lengo ni kuwapa afueni wajasiriamali wadogo wanaotegemea vyombo hivi katika kujipatia kipato, sambamba na kuongeza ufanisi katika ukusanyaji wa mapato ya Serikali.
#bajetikuu2025
#azamnewsupdates
✍️@official_jennifersumi