Sera za kinafiki za Marekani kuhusu matumizi ya nishati ya nyuklia

Katika taarifa yake mpya kuhusu matumizi ya nishati ya nyuklia, Waziri wa Nishati wa serikali ya Marekani, Chris Wright, amesema kutokana na Marekani kuwa kinara katika masuala ya akili mnemba (artificial intelligence) na ili kuwashinda wapinzani katika teknolojia hii, nchi yake inahitaji kusambaza umeme kutoka kwenye vyanzo vya kuaminika na vya bei nafuu kama vile nishati ya nyuklia.