
Seneta wa Marekani Bernie Sanders ameunga mkono uamuzi uliotoloewa na Mahakama ya Kimataifa ya Jinai ICC jana Alkhamisi wa kuamuru kukamatwa waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu na waziri wa zamani wa vita wa utawala huo haramu Yoav Gallant.
Sanders ameeleza katika taarifa kwamba mashtaka ya ICC “yana msingi mzuri,” akisisitiza umuhimu wa Mikataba ya Geneva, ambayo iliundwa kulinda raia na kuzuia vitendo visivyo vya kibinadamu wakati wa vita.
Seneta huyo wa Marekani amesema, mashtaka ya ICC dhidi ya Netanyahu na Gallant kwa kufanya jinai ikiwemo kutumia njaa kama silaha na kuwalenga raia ni ya haki.
Amefafanua kwa kusema: “ikiwa dunia haitazingatia sheria za kimataifa, tutaingia kwenye ushenzi zaidi”. “Nakubaliana na maamuzi ya ICC.”
Katika hatua ya kihistoria, Mahakama ya Kimataifa ya Jinai yenye makao yake The Hague imetangaza kuwa imetoa hati za kukamatwa viongozi hao wawili wa utawala wa Kizayuni kwa kuhusika na uhalifu wa kivita katika maeneo ya Wapalestina ukiwemo Ukanda wa Ghaza…/