Seneta Colombia angali mahututi baada ya kupigwa risasi

Haya ni kulingana na hospitali anayopokea matibabu.

“Tunaendelea kuchukua hatua kukabiliana na hatari inayoweza kutokana na majeraha aliyoyapata,” ilisema taarifa ya Hospitali ya Wakfu wa Santa Fe.

Uribe mwenye umri wa miaka 39 alipigwa risasi ya kichwa kwa karibu na miongoni mwa matibabu aliyofanyiwa ni upasuaji w aubongo.

Tukio hilo kupigwa kwake risasi lilifanyika wakati alipokuwa akilihutubia kundi dogo la watu waliokuwa wamekusanyika katika bustani ya Modelia huko Bogota.

Maafisa wa polisi katika eneo alikopigwa risasi seneta Uribe
Maafisa wa polisi katika eneo alikopigwa risasi seneta UribePicha: Raul Arboleda/AFP/Getty Images

Hapo Jumapili, mamia ya watu walikusanyika nje ya hospitali anayotibiwa Uribe ili kumfanyia maombi aweze kupona. Baadhi ya hao waliokusanyika walikuwa wakiimba nyimbo za kumpinga Rais Gustavo Petro.

Rais Petro mwenyewe amelaani tukio hilo na kutoa wito kwa wapinzani wake wasilitumie kwa ajili ya manufaa ya kisiasa. Ila baadhi ya Wacolombia pia wamemtaka rais huyo kupunguza matamshi yake ya kuwakosoa wanasiasa wa upinzani.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *