Senegal: Ziara ya Ousmane Sonko nchini Burkina Faso yakosolewa vikali

Kufuatia ziara ya kirafiki na kikazi ya Waziri Mkuu wa Senegal Ousmane Sonko nchini Burkina Faso siku ya Ijumaa tarehe 16 na Jumamosi tarehe 17 Mei 2025 , nchi hizo mbili zilisisitiza umuhimu wa kuimarisha ushirikiano wao, hasa katika sekta ya usalama na uchumi. Lakini ziara hii katika nchi inayoongozwa na wanajeshi waliofanya mapinguzi ambao wamevunja uhusiano wao na ECOWAS na kujiunga na AES (iliyoundwa na Niger na Mali) pia inazua mojaya maswali kuhusu ufaafu wa mbinu hiyo.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Na mwanahabari wetu huko Dakar, Gwendal Lavina

Baadhi ya vyama vya kiraia vya Senegal na upinzani wanahofia uhalali kamili wa mamlaka ya Burkina Faso iliyoingia madarakani kupitia mapinduzi ya kijeshi. Yoro Dia, mwanasayansi wa siasa na msemaji wa zamani wa rais chini ya urais wa Macky Sall, ambaye anakosoa sana ziara hiyo, hata anaiita kuwa ni makosa ya kisiasa kwa upande wa Waziri Mkuu: “Sote tunakubali kwamba uwezo lazima unganishwe. Lakini kupambana na ugaidi kunamaanisha kwanza kabisa kuwa na mamlaka halali. Senegal inapaswa kuwa na msimamo sahihi na kuyaambia mataifa ya ESA kwa udugu wote kwamba suluhu pekee leo ni kurejea kwa demokrasia na kwamba watu huru waamue mwelekeo wanaotaka kutoa kwa siku zijazo. “

Serikali na Pastef wanabaini kwamba ni kwa kwenda Ouagadougou ndio mambo yanaweza kusonga mbele na sio kuendelea kutumia sera ya ECOWAS ya kujitenga. Amadou Ba, Mbunge wa Pastef anasema: “Mkakati huu umeonyesha ukomo wake. Mwishowe, vikwazo hivi havikuleta athari yoyote isipokuwa athari mbaya kwa raia. Sasa, Senegal tuan mbinu mpya, na Rais Bassirou Diomaye Faye amekuwa na mtazamo wa usawa na uwajibikaji kila wakati kuhakikisha kwamba tunapata ratiba ya upatanishi, kanuni na maazimio ili nchi hizi ziweze kurejea viwango vya kidemokrasia.”

Ishara nyingine ya kufugua uhusiano: nia ya kuandaa hivi karibuni kikao cha 6 cha Tume ya Ushirikiano Mkuu wa Pamoja kati ya Burkina Faso na Senegal.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *