
Wakati Senegal ikiadhimisha Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani leo Jumamosi, Mei 3, mjadala unaibua taharuki nchini humo.
Imechapishwa:
Dakika 2
Matangazo ya kibiashara
Na mwandishi wetu wa habari huko Dakar, Léa-Liza Westerhoff
Je, kusimamishwa kwa vyombo vya habari ambavyo havikidhi mahitaji ya kiutawala ya Kanuni ya Vyombo vya Habari kunajumuisha shambulio dhidi ya uhuru wa vyombo vya habari? Ndiyo, wanajibu waandishi wa habari ambao wana wasiwasi kuhusu kupigwa marufuku uchapishaji wa makala kwa vyombo vya habari 381 ambavyo vimeshindwa kufikia vigezo vinavyohitajika na kanuni ya vyombo vya habari. Hapana, inasema Wizara ya Mawasiliano, ambayo inahakikisha kwamba inataka kusafisha sekta hiyo.
Habibou Dia, mkurugenzi wa mawasiliano katika Wizara ya Mawasiliano ya Senegal, anahakikisha kuwa kusimamisha vyombo vya habari 381 ambavyo havizingatii matakwa ya kiutawala ya kanuni za vyombo vya habari kutaleta utulivu katika sekta ambayo imekuwa haitimizi vigezo vyake.
Leo, wadau wana haja ya kusema juu ya kufungwa kwa vyombo vya habari. Lakini hakuna ofisi za vyombo hivyo vya habari zilizofungwa.
Lakini kwa rais wa chama cha waajiri wa vyombo vya habari nchini Senegal anasema hili ni shambulio dhidi ya wingi wa vyombo vya habari, na mamlaka inatumia vibaya mamlaka yake, kulingana na Mamadou Ibra Kane. “Kama waziri atachukua haki ya kusema ni nani bora, afuate au la, huo ni ukiukwaji wa uhuru wa vyombo vya habari, hauko ndani ya uwezo wake.”
“Vigezo ambavyo havifai tena”
Tatizo jingine ni kwamba vigezo vilivyowekwa na kanuni ya vyombo vya habari havikubaliwi tena kwa mazingira ya sasa ya vyombo vya habari. Kabla ya kuwekewa vikwazo, ingekuwa vyema kuifanyia marekebisho, anabaini Moussa Ngom, vyombo vya habari vinavyojihusisha na masuala ya uchunguzi wa kina ambavyo anaongoza havikidhi vigezo na sheria. “Kanuni ya vyombo vya habari imekuwepo tangu mwaka 2017. Wizara inaweza kujiwekea kikomo kwa kutotumia, kwa wakati huu, masharti ambayo ni vikwazo sana, na kuanza kurekebisha kanuni ya vyombo vya habari. Sasa, ikiwa serikali ya Senegal inataka kutuwekea vikwazo, angalau vikwazo hivi vitafungua macho ya kila mtu kwa kipengele cha matatizo ya kanuni ya vyombo vya habari.”
Kufikia sasa, karibu vyombo hamsini vya habari vimearifiwa kuhusu kusimamishwa kwao. Hofu ni kwamba uamuzi huu hatimaye utazuia uhuru wa habari wa raia wa Senegal. Wizara ya Mawasiliano hata hivyo imesisitiza kuwa vyombo vya habari vilivyosimamishwa bado vina chaguo la kutii sheria kwenye jukwaa la mtandaoni lililowekwa.