Senegal: Rais wa zamani Macky Sall kuitishwa mahakamani

Rais wa zamani wa Senegal Macky Sall, ambaye aliongoza Senegal kutoka mwaka 2012 hadi mwaka 2024, “ataitishwa mahakamani” kwa “vitendo vyake vibaya” katika usimamizi wa nchi, imesema serikali, ambayo inamtuhumu kuwajibika kwa “takwimu za uwongo” zilizofichuliwa katika ripoti ya fedha za umma.

Imechapishwa:

Dakika 3

Matangazo ya kibiashara

Iwapo mashtaka yatafunguliwa dhidi ya Bw Sall, itakuwa mara ya kwanza kwa mkuu wa zamani wa nchi kufikishwa mahakamani kujibu tuhuma zinahusu wadhifa wake wa zamani tangu Senegal, nchi inayojulikana kwa demokrasia, kupata uhuru wake mwaka 1960. Tangu mwezi Aprili, Senegal imekuwa ikiongozwa na serikali mpya ambayo inatetea uhuru na kuvunja mfumo huo. “Bila shaka, Macky Sall atakabiliwa na sheria. Yeye ndiye mtu wa kwanza kuhusika na vitendo vibaya vilivyofanywa,” msemaji wa serikali ya Senegal Moustapha Ndjekk Sarré alisema siku ya Ijumaa kwenye kituo cha redio cha kibinafsi cha RFM.

“Simpi nafasi ya kujitetea kwa sasa. Kila kitu kilichotokea kilifanyika chini ya maagizo yake. Anaweza hata kuchukuliwa kuwa kiongozi wa genge lililofanya vitendo vya uhalifu. Kesi za kisheria haziwezi kuepukika,” alisema Bw. Sarré, ambaye pia ni Waziri wa Mafunzo ya Ufundi. Alihojiwa hasa baada ya Rais Sall siku ya Alhamisi kukosoa ripoti iliyochapishwa tarehe 12 Februari na Mahakama ya Ukaguzi wa Hesabu, hati ambayo inatilia shaka serikali ya zamani katika usimamizi wa fedha za umma.

“Mahakama ya Ukaguzi wa Hesabu kwa hakika ni mojawapo ya taasisi zinazoaminika zaidi katika Jamhuri yetu ambayo imeidhinisha ukaguzi (wa umma). Anachohitajika kufanya ni kuomba msamaha,” alisema Bw Sarré. “Nimesalia na imani kuwa yeye anahusika na vitendo hivi vyote ambavyo vimeelezewa katika ukaguzi,” aliongeza.

Kiongozi huyo wa zamani “ana kinga ya kufauatilia na vyombo vya sheria kama Rais (wa zamani) wa Jamhuri. Tuna mfumo huru wa haki. Ikiwa haki itagundua kwamba hajafanya lolote, hatasalimika,” alisema Waziri Sarré.

Mwishoni mwa mwezi Desemba, Bunge lilianzisha Mahakama Kuu ya Haki, mamlaka iliyoanzishwa mwanzoni mwa kila bunge ambapo Rais wa Jamhuri na wajumbe wa serikali wanaweza kuhukumiwa kwa “uhaini mkubwa”. Taasisi huru ya ukaguzi, Mahakama ya Ukaguzi ilisisitiza kwamba viteno vilivyoripotiwa katika ripoti yake “vinafikiriwa kuwa ni usimamizi mbaya, usimamizi wa vite,do au makosa ya jinai”. Deni ambalo halijalipwa linawakilisha 99.67% ya Pato la Taifa, kiwango “cha juu” kuliko kiasi kilichotangazwa na serikali iliyopita, kulingana na ripoti.

Nakisi ya bajeti “iliyohesabiwa upya” na Mahakama kwa mwaka wa 2023 ni, kwa mfano, 12.3% dhidi ya 4.9% iliyotangazwa. Bw. Sall, ambaye anaishi Morocco tangu kuondoka madarakani, alikosoa ripoti hii kutoka kwa Mahakama ya Ukaguzi wa Hesabu katika mahojiano yaliyochapishwa siku ya Alhamisi na Gazeti la Jeune Afrique (JA). “Ninakataa kabisa madai haya ya uwongo,” Bw. Sall alisema katika mahojiano haya. “Ni mchakato wa kisiasa. Daima tumefanya kazi kwa uwazi kabisa na washirika wote. Kila mwaka, Mahakama ya ukaguzi imeidhinisha hesabu za fedha za taiafa la Senegal. Ni rahisi sana kurudi baadaye na kusema kwamba yote haya yalikuwa ya uongo. Yote haya ni ujinga,” alisema.

Mnamo mwezi Septemba, serikali ya Senegal ilishutumu serikali ya zamani kwa kuzalisha “takwimu za uongo” za madeni na hasa nakisi ya bajeti. “Siogopi chochote,” Macky Sall alisema, kabla ya kuongeza: “Wanaweza kuendelea ikiwa wanataka.” Mnamo Februari 13, mamlaka mpya ya Senegal ilitangaza uwezekano wa kesi za kisheria dhidi ya wahusika wa “makosa makubwa” yaliyofichuliwa na Mahakama ya Ukaguzi. Pia walitangaza katika siku zijazo kufutwa kwa sheria ya msamaha, inayohusu ukweli unaohusiana na ghasia za kisiasa kati ya mwaka 2021 na 2024. Sheria hii ilipitishwa mwezi Machi mwaka uliyopita kwa mpango wa rais wa zamani Sall na kabla ya uchaguzi wa urais ambao Rais Bassirou Diomaye Faye aliibuka mshindi mwishoni mwa mwezi Machi